• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 21, 2014

  CAF YAIENGUA GAMBIA KWA KUCHOMEKEA VIJEBA U20 MICHUANO YA AFRIKA

  KAMATI ya Maandalizi ya michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imeiengua timu ya Gambia kwenye mbio za kusaka tiketi ya kucheza fainali za michuano hiyo mwakani nchini Senegal.
  Uamuzi huo unafuatia malalamiko ya mapema ya Liberia juu ya baadhi ya wachezaji wa Gambia baada ya mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Jumapili ya Aprili 6 mwaka huu, ambao Gambia ilishinda 1-0.

  Wachezaji walioiponza Gambia ni Sampierre Mendy, Buba Sanneh, Bubacarr Trawally, Saloum Fall na Ali Sowe ambao wote  walizaliwa mwaka 1994 na hawastahili kucheza mashindano hayo yanayohitaji wachezaji waliozaliwa baada ya Januari 1 mwaka 1995, kama ilivyoelezwa katika barua zilizotumwa kwa nchi wanachama wote wa CAF Septemba 2, mwaka 2013.
  Kwa uamuzi huu, mechi namba 22 ya marudiano baina ya Gambia na Liberia iliyokuwa ipigwe kati ya Aprili 25 na 27 imefutwa na Liberia imefuzu hatua inayofuata.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CAF YAIENGUA GAMBIA KWA KUCHOMEKEA VIJEBA U20 MICHUANO YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top