• HABARI MPYA

    Tuesday, April 01, 2014

    MOYES AMUONYA REFA CARBALLO JUU YA KUJIRUSHA KWA ROBBEN MAN UTD IKIIVAA BAYERN LEO OLD TRAFFORD

    KOCHA wa Manchester United, David Moyes amemuambia refa wa Hispania, Carlos Carballo kutoa maamuzi sahihi katika mchezo wao dhidi ya mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich kutokana na tabia ya wachezaji wa timu hiyo kujirusha kujiangusha.
    United inatakutana na mabingwa wa Bundesliga leo Uwanja wa Old Trafford katika mchezo wa kwanza wa kwanza wa Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya. Bayern inapewa nafasi kubwa ya kushinda, lakini timu hiyo ya kocha Pep Guardiola ilishutumiwa baada ya kuitoa Arsenal katika raundi iliyopita, kwa Arsene Wenger kumlaumu Arjen Robben kuwa hodari wa kujirusha kujiangusha.
    Moyes alisema: "Tunawaamini marefa watafanya uamuzi sahihi. Kujirusha ni moja ya vitu vibaya vya kufanyia kazi. Ningependa kutahadharisha juu ya hilo, lakini nisingependa kumlenga mchezaji binafsi,".

    Winga Mholanzi Anayepaa: Nyota wa Bayern, Arjen Robben amekuwa akishutumiwa kwa kujiangusha kirahisi
    Wishlist: Manchester United boss David Moyes hopes referee Carlos Velasco Carballo punishes diving
    Angalizo la tahadhari: Kocha wa Manchester United, David Moyes anatumai refa Carlos Velasco Carballo atwaadhibu wachezaji wa kujiangusha

    United imekuwa ikiumizwa na maamuzi ya marefa siku za karibuni katika michuano ya Ulaya, na winga Nani alitolewa kwa kadi nyekundu dhidi ya Real Madrid mwaka jana wakati beki Rafael alitolewa pia dhidi ya Bayern mwaka 2010. 
    Wajerumani hao tayari wamekwishatetea ubingwa wa Bundesliga na wameshinda mechi zao 27 kati ya 30 zilizopita kwenye mashindano yote. Lakini Ryan Giggs bado anaamini United inaweza kufika fainali.
    Flashpoint: Arsene Wenger criticised Robben for this incident with Wojciech Szczesny in the last round
    Muongo mkubwa: Arsene Wenger alimshutumu Robben kwa tukio hili alipojiangusha wakati alipokutana na kipa Wojciech Szczesny katika raundi iliyopita
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MOYES AMUONYA REFA CARBALLO JUU YA KUJIRUSHA KWA ROBBEN MAN UTD IKIIVAA BAYERN LEO OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top