• HABARI MPYA

    Sunday, December 01, 2013

    BALE APIGA HAT-TRICK REAL IKIUA 4-0 NA KUISOGELEA BARCA MGONGONI KABISA LA LIGA

    WINGA Gareth Bale jana amefunga mabao matatu peke yake yaani hat-trick wakati Real Madrid ikiitandika Valladolid 4-0 Uwanja wa Bernabeu, Madrid na kuisogelea Barcelona kileleni mwa La Liga ikibaki inazidiwa pointi tatu.
    Mchezaji huyo ghali wa dunia ameendelea kutekeleza vyema majukumu ya Cristiano Ronaldo ambaye ni majeruhi kwa sasa akiwa ametimiza mabao tisa katika mechi 13.Bale aliyefunga mabao hayo katika dakika za 33, 64 na 89 huku lingine liifungwa na Karim Benzema dakika ua 36, anakuwa mchezaji wa pili wa Uingereza kufunga hat-trick katika La Liga akimfuatia Gary Lineker mwaka 1987.
    Real Madrid: Lopez, Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo, Alonso, Modric, Di Maria, Isco, Bale na Benzema.
    Real Valladolid: Marino, Alcatraz, Rueda, Valiente, Pena, Rubio, Sastre, Rossi, Larsson, Guerray na Bergdich.
    La kwanza: Winga wa Real Madrid, Gareth Bale akishangilia bao lake la kwanza Uwanja wa Bernabeu jana
    Stuck in: Bale vies for possession with Valladolid's forward Javi Guerra
    Bale akimtoka mshambuliaji wa Valladolid, Javi Guerra
    Tight at the top: Bale helped Real Madrid narrow the gap at the top of La Liga to three points
    Bale ameisaidia Real Madrid kupunguza la pointi La Liga wanazozidiwa na vinara Barcelona hadi kubaki tatu
    Gary Lineker's tweet to Gareth Bale

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BALE APIGA HAT-TRICK REAL IKIUA 4-0 NA KUISOGELEA BARCA MGONGONI KABISA LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top