• HABARI MPYA

  Sunday, November 04, 2018

  MBWANA SAMATTA ADHIBITIWA KRC GENK YALAZIMISHWA SARE 1-1 NA CLUB BRUGGE LIGI YA UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana alicheza kwa dakika zote 90, timu yake, KRC Genk ikilazimishwa sare ya 1-1 na Club Brugge katika mchezo wa nyumbani wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
  Genk walianza vizuri kwa bao la mshambuliaji kutoka DRC, Dieumerci N'Dongala dakika ya 10, kabla ya mshambuliaji Mbelgiji, Siebe Schrijvers kuisawazishia Brugge dakika ya 53.
  Kwa Samatta jana amefikisha mechi 127 katika mashindano yote tangu amejiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na amefunga jumla ya mabao 51.

  Mbwana Samatta (kulia) akimpomeza Dieumerci N'Dongala baada ya kufingua bao la pii Genk jana

  Katika Ligi ya Ubelgiji amecheza mechi 99 na kufunga mabao 36, Kombe la Ubelgiji mechi nane mabao mawili na Europa League mechi 20 mabao 14.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa; Vukovic, Maehle, Aidoo, Dewaest, Uronen, Heynen, Berge/Wouters dk62, Malinovskyi, Pozuelo, Ndongala/Zhegrova dk73 na Samatta.
  Club Brugge; Horvath, Poulain, Wesley, Diatta/Cools dk82, Writers/Vormer dk71, Nakamba/Ambrabat dk90+2, Vanaken, Denswil, Rits, Mechele na Mata.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBWANA SAMATTA ADHIBITIWA KRC GENK YALAZIMISHWA SARE 1-1 NA CLUB BRUGGE LIGI YA UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top