• HABARI MPYA

  Thursday, November 15, 2018

  BMT YANDAA MASHINDANO YA RIADHA YA WANAWAKE KWA KUSHIRIKIANA NA JICA YATAFANYIKA NOVEMBA 24 NA 25 DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BARAZA LA michezo la  Taifa (BMT),  kwa kushirikiana na Taasisi ya Ushirikiano wa Kimataifa WA Japan (JICA), wameandaa tena mashindano ya raidha kwa wanawake yatakayojulikana kama 'Ladies First'. 
  Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Novemba 24 na 25 mwaka huu, kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salama. 
  Akizungumza na Waandishi wa Habari jana mjini Dar es Salaam, Afisa Habari wa BMT, Najah Bakari alisema kuwa lengo kuu la mashindano hayo ni kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika mchezo wa riadha ili waweze kupata fursa ya ajira pamoja na kuiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa ikiwemo 2020 Olympiki Tokyo Japan. 
  Najah alisema kuwa mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani inahamasishwa kwa kuwakilishwa na wanariadha wanne na kiongozi mmoja, tunatarajia kuwa na wanamichezo 155 katika mbio hizo. 
  "Sisi kama BMT tunapenda kuvikumbusha vyama vya riadha ngazi za mikoa kwa kushirikiana na kamati zao za michezo kwa kuchagua timu na kuzisafirisha kuja kwenye mashindano haya, "alisema Najah
  Naye muwakilishi mkuu wa JICA, Takusaburo Kimuro, amesema kuwa hadi sasa mikoa 27 tayari imeshathibitisha kushiriki mashindano hayo ikiwemo na Simiyu,  Singida,  Mbeya, Arusha, Dodoma,  Tanga. 
  Mingine ni Njombe, Kagera, Iringa, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Morogoro, Mwanza Pwani, Lindi, Mara, Manyara, Rukwa, Geita, Mtwara na Ruvuma.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BMT YANDAA MASHINDANO YA RIADHA YA WANAWAKE KWA KUSHIRIKIANA NA JICA YATAFANYIKA NOVEMBA 24 NA 25 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top