• HABARI MPYA

  Tuesday, January 05, 2016

  ZIDANE AAHIDI KUIPA TAJI REAL MADRID, ASEMA ATAPIGA 'MZIGO WA KUFA MTU"

  KOCHA mpya, Zinedine Zidane ameahidi kushinda taji msimu huu baada ya kuchukua nafasi ya Rafael Benitez Real Madrid.
  Mwanasoka huyo bora wa zamani wa dunia mwenye umri wa miaka 43, mshindi wa Kombe la Dunia na mchezaji wa zamani wa, Real na Ufaransa ametambulishwa jana na Rais, Florentino Perez kufuatia kuondolewa Benitez baada ya kuingoza timu katika mechi 25.
  Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari jana, Zidane alisema; "Nataka kuishukuru klabu na kumshukuru Rais kwa kunipa fursa ya kufundisha klabu hii,".
  Gwiji wa soka, Zinedine Zidane akizungumza na Waandishi wa Habari jana baada ya kutambulishwa kuwa kocha mpya wa Real Madrid PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  "Ni klabu bora duniani na yenye mashabiki wengi duniani. Nataka kufanya mazuri sana kuhakikisha kwamba klabu hii mwishoni mwa msimu inapata taji. Nitafanya kazi kwa bidii na wachezaji wote na ninafikiri itakwenda vizuri. Najiandaa kufanya kazi na kila mtu," amongeza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZIDANE AAHIDI KUIPA TAJI REAL MADRID, ASEMA ATAPIGA 'MZIGO WA KUFA MTU" Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top