• HABARI MPYA

  Sunday, July 02, 2023

  NI MTIBWA SUGAR MABINGWA TENA WA LIGI KUU YA VIJANA U20  TIMU ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vijana kwa mara ya tano mfululizo baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo uliodumu kwa dakika 120 leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Bao pekee la Mtibwa Sugar U20 ya kocha Awadh Juma limefungwa na mshambuliaji wake tegemeo, Athumani Makambo dakika ya 97 na kuzima ndoto ya Vijana wa Choke Abeid kubeba taji la kwanza la michuano hiyo.
  Mapema katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu, Azam FC iliichapa Kagera Sugar 3-1 hapo hapo Azam Complex.
  Mabao yote ya Azam FC ya kocha Mohamed Badru yamefungwa na Cyprian Kachwele dakika za 22, 27 na 45 na ushei, wakati la Kagera Sugar ya kocha Vincent Barnabas limefumgwa na Hussein Kombo dakika ya 90 na ushei.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI MTIBWA SUGAR MABINGWA TENA WA LIGI KUU YA VIJANA U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top