![]() |
| Kwaheri Manyika Peter Manyika, pumzika kwa amani kipa hodari na mahiri. |
KIPA wa zamani wa Kimataifa wa Tanzania, Manyika Peter Manyika (52) amefariki dunia Alfajiri ya leo Jijini Dar es Salaam.
Manyika ambaye ni baba wa kipa wa zamani wa Simba SC Peter Manyika Junior - mwili wake umehifadhiwa katika hospital ya Mwananyamala, Dar es Salaam huku taratibu za mazishi zikiendelea.
Manyika aliibukia Mapipa Rangers ya Magomeni Mapipa, kabla ya kwenda MtoSingida, Mtibwa Sugar ikiwa Daraja la Tatuakaipandisha Ligi Kuu mwaka 1996, kabla yakuhamia Sigara FC ya Dar es Salaam ambakoalidumu kwa msimu mmoja, 1997.
![]() |
| Huyu ni mwanawe, Peter Manyika ambaye alidakia kwa mahasimu, Simba SC |
Akiwa Sigara aliiponza timu hiyo kushushwaDaraja baada ya kupokwa pointi za mechi zotealizodaka kwa sababu ya ukiukwaji wa taratibuza usajili wake kutoka Mtibwa Sugar.
Mwaka 1998 alijiunga na Yanga SC ambako aliidakia hadi mwaka 2000 akaenda Falme zaKiarabu (UAE), kuchezea Adma FC kwa miezi kadhaa, akarejea mwaka 2001 na kucheza kwa msimu mmoja, kabla ya kwenda Shelisheli, baadaye Vietnam, Afrika Kusini, Botswana na Namibia kuchezea timu mbalimbali – kabla ya kurejea nchini kumalizia soka yake katika timu ya Villa Squad mwaka 2006 na kujikita kwenye Ukocha wa Makipa kufuatia kusomeshwa na TFF nchini Afrika Kusini.
![]() |
| Manyika Peter kabla ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1998 dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco uliomalizika kwa sare ya 3-3 Uwanja wa Taifa, sasa Uhuru, Dar es Salaam |
![]() |
| Manyika Peter hapa Yanga ikimenyana na Zamalek ya Misri katika mechi ya Kombe la Washindi Afrika liomalizika kwa sare ya 1-1 Uwanja wa Taifa, sasa Uhuru, Dar es Salaam |
Manyika pia alikuwa kipa namba moja wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kati ya mwaka 1998 na 2002 alipopokonywa namba na Juma Kaseja.
Baada ya kistaafu soka, pamoja na Ukocha lakini pia Manyika alikuwa anajishughulisha na muziki.
Mungu ampumzishe kwa amani. 😭
![]() |
| Manyika Peter mwenye kofia kabla ya mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia ambao Taifa Stars ilifungwa 1-0 na Ghana mwaka 2001 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. |







.png)
0 comments:
Post a Comment