• HABARI MPYA

  Monday, July 03, 2023

  AZAM FC YATAMBULISHA MAKOCHA WAWILI KWA MPIGO


  KLABU ya Azam FC imetambulisha wataalamu wawili wapya wa benchi la ufundi, Kocha wa Makipa Khalifa Ababakar Fall na Ibrahim Diop ambaye ni Mchambuzi wa mechi (Video Analyst).
  Wawili hao wanaungana na Msenegal mwenzao, Youssouph Dabo ambaye ndiye Kocha Mkuu mpya wa Azam FC na wote wamesaini mkataba wa miaka mitatu kila mmoja.
  Ikumbukwe Azam FC ilibomoa benchi lake la Ufundi kwa kuwaondoa Kaimu Kocha Mkuu, Kali Ongala, Msaidizi wake, Aggrey Morris, Kocha wa Makipa, Mspaniola Dani Cadena na kocha wa Fiziki, Mtunisia Dk. Moadh Hiraoui.
  Azam pia imeacha wachezaji sita hadi sasa, ambao ni kipa Wilbol Maseke, mabeki Mzimbabwe Bruce Kangwa, Mkenya, Kenneth Muguna, Cleophace Mkandala kiungo Ismail Aziz na mshambuliaji Mzambia, Rodgers Kola, huku ikisajili viungo wawili tu, Mzanzibari Feisal Salum na Mgambia Gibrill Sillah.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YATAMBULISHA MAKOCHA WAWILI KWA MPIGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top