• HABARI MPYA

  Wednesday, July 05, 2023

  AZAM FC YALETA KOCHA MFARANSA KUMSAIDIA MSENEGAL


  KLABU ya Azam imemtambulisha Mfaransa, Bruno Ferry kuwa Kocha wake Msaidizi muda mfupi tu baada ya kuwasili nchini tayari kwa majukumu yake mapya.
  Sasa benchi la Ufundi la Azam FC linaundwa na Kocha Mkuu, Msenegal Youssouph Dabo, Kocha Msaidizi, Bruno Ferry, Kocha wa Makipa Khalifa Ababakar Fall na Ibrahim Diop ambaye ni Mchambuzi wa mechi (Video Analyst) wote kutoka Senegal pia.
  Bruno Ferry (56) ambaye enzi zake alikuwa kipa nchini Ufaransa ni Kocha mwenye uzoefu mkubwa ambaye amefundisha klabu mbalimbali zikiwemo Eding Sport FC ya Cameroon, Accra Lions ya Ghana na Louh.-Cuiseaux ya kwao, Ufaransa kama Kocha Mkuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YALETA KOCHA MFARANSA KUMSAIDIA MSENEGAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top