• HABARI MPYA

  Friday, May 05, 2023

  WYDAD YAAJIRI KOCHA WA ZAMANI WA SIMBA VANDENBROECK  MABINGWA wa Afrika, Wydad Club Athletic ya Morocco wamemuajiri Mbelgiji, Sven Ludwig Vandenbroeck kuwa kocha wake mpya Mkuu kufuatia kuachana na Mspaniola, Juan Carlos Garrido aliyedumu kwa miezi na ushei.
  Vandenbroeck alikuwa kocha wa Simba kwa mafanikio katí ya 2019 na 2021 akiipa mataji mfululizo na kuifikisha Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kabla ya kutimkia FAR Rabat ya Morocco pia na baadaye Abha FC ya Saudi Arabia.
  Wydad haijapata kocha wa kumuamini tangu kuondoka kwa  Walid Regragui aliyewapa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kuhamia timu ya taifa ya Morocco ambayo aliifikisha Nusu Fainali ya Kombe la Dunia mwaka jana Qatar.
  Tangu aondoke Regragui Walid imeajiri makocha wanne jumla hadi sasa, mbali na Garrido na Vandenbroeck, wengine ni Mmorocco Hussein Ammouta na Mtunisia Mehdi Nafti.
  Wydad tayari ipo Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuitoa kwa mbinde Simba SC kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya jumla ya 1-1 kila timu ikishinda 1-0 kwake.
  Katika Nusu Fainali itamenyana na timu ngumu kutoka Afrika Kusini, mechi ya kwanza ikichezwa Casablanca Mei 13 na marudiano Mei 20 Johannesburg.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WYDAD YAAJIRI KOCHA WA ZAMANI WA SIMBA VANDENBROECK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top