• HABARI MPYA

  Saturday, May 06, 2023

  WIZARA YAPOKEA TAARIFA YA HITILAFU YA UMEME UWANJA WA MKAPA


  WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Mei 6, 2023 akiwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, amepokea taarifa ya Kamati aliyoiunda kuchunguza tukio la kukatika umeme katika uwanja huo wakati wa mechi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati Timu ya Yanga na Rivers United ya Nigeria.
  Baada ya kupokea taarifa hiyo, Waziri Dkt. Chana amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg. Saidi Yakubu kufanyia kazi taarifa hiyo ikiwemo kuchukua hatua zinazostahili kulingana na taarifa hiyo. Tukio hilo la kupokea taarifa lilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu,Bw Nicholaus Mkapa.
  Kamati hiyo imeongozwa na Mwenyekiti Mhandisi Keneth Boymanda kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), ikiwa na Wajumbe kutoka Wakala wa Majengo nchini TBA, na baadhi ya watumishi wa Wizara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WIZARA YAPOKEA TAARIFA YA HITILAFU YA UMEME UWANJA WA MKAPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top