• HABARI MPYA

  Saturday, May 06, 2023

  KITAYOSCE NA PAMBA ZOTE ZASHINDA 1-0 NYUMBANI CHAMPIONSHIP


  TIMU za Pamba na Kitayosce zinazowania nafasi ya mwisho ya kupanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao leo zote zimepata ushindi wa 1-0 zote nyumbani katika Ligi ya Championship.
  Wakati Kitayosce imeichapa 1-0 Mbuni ya Arusha Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora, nayo Pamba imeibuka na ushindi wa 1-0 pia dhidi ya mabingwa wa Championship tayari, JKT Tanzania Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
  Mechi nyingine ya leo za Championship, wenyeji Ken Gold wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Copco FC ya Mwanza Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.
  Msimamo wa Championship sasa JKT Tanzania pointi 63 mechi 28, Kitayosce pointi 57 na Pamba pointi 56 baada ya wote kucheza mechi 27 kuelekea mechi tatu za mwisho za kuamua timu ya pili ya kupanda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KITAYOSCE NA PAMBA ZOTE ZASHINDA 1-0 NYUMBANI CHAMPIONSHIP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top