• HABARI MPYA

  Monday, May 08, 2023

  WEST HAM YAIPIGA KIDUDE MAN UNITED


  WENYEJI, West Ham United wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa London.
  Bao pekee la West Ham United limefungwa na mshambuliaji Mualgeria, Mohamed Saïd Benrahma aliyemtungua kipa David de Gea kwa shuti la umbali wa mita 20 dakika ya 27.
  Kwa ushindi huo, West Ham United ya kocha David Moyes inafikisha pointi 37 katika mchezo wa 35, ingawa inabaki nafasi ya 15, wakati Manchester United inabaki na pointi zake 63 za mechi 34 nafasi ya nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WEST HAM YAIPIGA KIDUDE MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top