• HABARI MPYA

  Monday, May 08, 2023

  ARSENAL YAWABUTUA NEWCASTLE UNITED 2-0 ST JAMES PARK  TIMU ya Arsenal imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa St. James' Park, Newcastle upon Tyne.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Martin Odegaard dakika ya 14 na Fabian Schar aliyejifunga dakika ya 71.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 81 katika mchezo wa 34 ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na mabingwa watetezi, Manchester City, ambao pia wana mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao, Newcastle United inabaki pointi zake 65 za mechi 34 nafasi ya tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAWABUTUA NEWCASTLE UNITED 2-0 ST JAMES PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top