• HABARI MPYA

  Saturday, May 06, 2023

  MAN CITY YAICHAPA LEEDS UNITED 2-1 NA KUKAA SAWA KILELENI


  MABINGWA watetezi, Manchester City wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Leeds United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad.
  Mabao ya Manchester City leo yamefungwa na kiungo Mjerumani Ilkay Gundogan dakika ya 19 na 27 mara zote akimalizia pasi za Mualgeria, Riyad Mahrez, wakati la Leeds limefungwa na Rodrigo dakika ya 85.
  Ilkay Gundogan angeweza kuondoka na mpira leo kama si kukosa mkwaju wa penalti dakika y 84.
  Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 82 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi nne zaidi ya Arsenal baada ya wote kucheza mechi 34, wakati Leeds United inabaki na pointi zake 30 za mechi 35 nafasi ya 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAICHAPA LEEDS UNITED 2-1 NA KUKAA SAWA KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top