• HABARI MPYA

  Saturday, May 06, 2023

  CHELSEA YASHINDA MECHI YA KWANZA TANGU LAMPARD AREJEE


  HATIMAYE Kocha Frank Lampard amepata ushindi wa kwanza tangu arejee Chelsea baada ya leo kuichapa Bournemouth mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Vitality, Bournemouth, Dorset.
  Mabao ya Chelsea yamefungwa na Conor Gallagher dakika ya tisa,
  Benoit Badiashile dakika ya 82 na  Joao Felix dakika ya 86, wakati la Bournemouth limefungwa na Matias Vina dakika ya 21.
  Kwa ushindi huo Chelsea inafikisha pointi 42 katika mchezo wa 34 na kusogea nafasi ya 11, wakati Bournemouth inabaki na pointi zake 39 za mechi 35 nafasi ya 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YASHINDA MECHI YA KWANZA TANGU LAMPARD AREJEE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top