• HABARI MPYA

  Thursday, May 04, 2023

  AZIZ KI NA MZIZE WAFUNGA YANGA YAICHAPA SINGIDA 2-0 LITI


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wamebakiza pointi tatu tu kutawazwa kuwa mabingwa tena wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa msimu wa pili mfululizo.
  Hiyo ni baada ya ushindi wa 2-0, mabao ya Mburkinabe, Stephanie Aziz Ki dakika ya 15 na chipukizi Clement Francis Mzize dakika ya 21 leo dhidi ya wenyeji, Singida Big Stars Uwanja wa LITI mjini Singida.
  Yanga imefikisha pointi 71 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi saba zaidi ya watani wao, Simba baada ya wote kucheza mechi 27 kuelekea mechi tatu za mwisho.
  Singida Big Stars inabaki na pointi zake 51 nafasi ya nne, ikizidiwa pointi mbili na Azam FC walio nafasi ya tatu baada ya wote kucheza mechi 27.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZIZ KI NA MZIZE WAFUNGA YANGA YAICHAPA SINGIDA 2-0 LITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top