• HABARI MPYA

  Saturday, April 08, 2023

  MAYELE AIPELEKA YANGA NUSU FAINALI KOMBE LA TFF


  MSHAMBULIAJI Mkongo, Fiston Kalala Mayele ametokea benchi kuifungia Yanga bao pekee ikiichapa Geita Gold 1-0 na kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mayele alifunga bao hilo dakika ya 57 akimalizia pasi ya Mkongo mwenzake, winga Tuisila Kisinda baada ya kuingia mwanzoni tu mwa kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Clement Mzize.
  Yanga sasa itakutana na Singida Big Stars katika Nusu Fainali ya ASFC mwishoni mwa mwezi huu, wakati Simba SC itamenyana na Azam FC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE AIPELEKA YANGA NUSU FAINALI KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top