• HABARI MPYA

  Friday, March 10, 2023

  MAN UNITED YAMALIZA HASIRA REAL, YAWAPIGA 4-1


  WENYEJI, Manchester United wamejiweka kwenye nafasi nzuri ya kwenda Robo Fainali ya UEFA Europa League kufuatia ushindi wa 4-1 dhidi ya Real Betis jana Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mabao ya Man United yalifungwa na Marcus Rashford dakika ya sita, Antony dakika ya 52, Bruno Fernandes dakika ya 58 na Wout Weghorst dakika ya 82, wakati la Real Betis limefungwa na Ayoze Pérez dakika ya 32.
  Timu hizo zitarudiana Machi 16 Uwanja wa Benito Villamarín Jijini Sevilla na mshindi wa jumla atakwenda Robo Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAMALIZA HASIRA REAL, YAWAPIGA 4-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top