• HABARI MPYA

  Friday, March 10, 2023

  ARSENAL YAPATA SARE KWA SPORTING 2-2 LISBON


  WENYEJI, Sporting Lisbon wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Arsenal katika mchezo wa kwanza Hatua ya 16 Bora michuano ya UEFA Europa League jana Uwanja wa José Alvalade Jijini Lisbon, Ureno.
  Mabao ya Sporting Lisbon yamefungwa na Gonçalo Inácio dakika ya 34 na Paulinho dakika ya 55, wakati ya Arsenal yamefungwa na William Saliba dakika ya 22 na Hidemasa Morita aliyejifunga dakika ya 63.
  Sasa timu hizo zitarudiana Machi 16 Jijini London na mshindi wa jumla atakwenda Robo Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAPATA SARE KWA SPORTING 2-2 LISBON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top