• HABARI MPYA

  Saturday, March 11, 2023

  BALEKE APIGA HAT TRICK SIMBA YAICHAPA MTIBWA 3-0 MANUNGU


  MSHAMBULIAJI Mkongo, Jean Baleke amefunga mabao yote matatu leo Simba SC ikiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mjini Morogoro.
  Baleke aliyesajiliwa dirisha dogo kwa mkopo kutoka TP Mazembe ya kwao, Lubumbashi alifunga mabao yake dakika ya tatu akimalizia pasi ya mshambuliaji mwenzake, Mzambia Moses Phiri, dakika ya saba kwa pasi ya kiungo Mrundi, Saido Ntibanzokiza na dakika ya 33 akimalizia pasi ya beki mzawa, Shomari Kapombe.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 57 katika mchezo wa 24, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tano na mabingwa watetezi, Yanga SC ambao pia wana mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao Mtibwa Sugar baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 29 za mechi 25 sasa nafasi ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BALEKE APIGA HAT TRICK SIMBA YAICHAPA MTIBWA 3-0 MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top