• HABARI MPYA

  Thursday, August 04, 2022

  YANGA YAICHAPA NAMUNGO 2-0 MECHI YA KIRAFIKI KIGAMBONI


  TIMU ya Yanga jana imeibuka na ushindi wa 2-0 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo FC Uwanja wa Avic Town, Somangira nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga yote yamefungwa na washambuliaji wake Wakongo, Heritier Makambo na Fiston Mayele kwa penalti na huo unakuwa mchezo wa tatu kwenye kambi yao ya kujiandaa na msimu, baada ya awali kushinda 6-1 dhidi ya Transit Camp na 9-0 dhidi ya Friends Rangers.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAICHAPA NAMUNGO 2-0 MECHI YA KIRAFIKI KIGAMBONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top