• HABARI MPYA

  Tuesday, May 03, 2022

  MAN UNITED YAICHAPA BRENTFORD 3-0 OLD TRAFFORD


  WENYEJI, Manchester United wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Brentford City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatatu Uwanja wa Old Trafford.
  Mabao ya Manchester United yamefungwa na Bruno Fernandes dakika ya tisa, Cristiano Ronaldo kwa penalti dakika ya 61 na Raphael Varane dakika ya 72 na kwa ushindi huo, Mashetani hao Wekundu wanafikisha pointi 58 katika mchezo wa 36, ingawa wanabaki nafasi ya sita wakizidiwa pointi tatu na Tottenham Hotspur ambayo pia ina mechi mbili mkononi.
  Brentford wao wanabaki na pointi zao 40 za mechi 35 nafasi ya 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAICHAPA BRENTFORD 3-0 OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top