• HABARI MPYA

    Wednesday, February 16, 2022

    PAMBA YATINGA ROBO FAINALI ASFC


    WENYEJI, Pamba FC imekuwa timu pekee ya daraja la chini ya Ligi Kuu Tanzania Bara kutinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji FC jioni ya leo Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
    Mabao ya Pamba, mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya Muungano nchini yamefungwa na Makiada Makoli dakika ya 15 na Masunga Malulu dakika ya 77, wakati la Dodoma Jiji FC limefungwa na Cleophace Mkandala dakika ya 47.
    Timu nyingine zilizofuzu Robo Fainali ni Azam FC iliyoichapa Baga Friends 6-0, Geita Gold iliyoichapa Mbuni FC 1-0, Coastal Union iliyoichapa Mtibwa Sugar 2-0, Kagera Sugar iliyoilaza Namungo FC 1-0, Polisi Tanzania iliyoipiga Tanzania Prisons 2-0 na Yanga SC iliyolaza Biashara United 2-1.
    Hatua ya 16 Bora ya ASFC itakamilishwa Saa 1:00 usiku leo kwa mchezo kati ya mabingwa watetezi, Simba SC na Ruvu Shooting Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PAMBA YATINGA ROBO FAINALI ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top