• HABARI MPYA

  Thursday, February 10, 2022

  FUNDI SELEMALA ASHINDA JACKPOT BONUS YA SPORTPESA.


  MKAZI wa Mbezi Beach Africana, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar-Es-Salaam John Willbaard Bugenyi, ameshinda shilingi 4,727,156, katika  Jackpot Bonus ya SportPesa iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyoisha, baada ya kupatia kwa usahihi mechi 11.
  Akizungumza baada ya makabidhiano ya mfano wa hundi katika ofisi za Sportpesa jijini Dar-Es-Salaam, John anasema alianza kucheza na Sportpesa miaka kadhaa iliyopita. ‘’Nilianza kucheza na Sportpesa kama sikosei miaka minne iliyopita’’.
  Kwa mujibu wake, John ambaye pia ni fundi selemala, anasema alivutiwa sana na jina la SportPesa  kabla ya rafiki yake mmoja kumtambulisha rasmi kwa kumuelekeza namna ya kucheza.
  ‘’Ujue nina rafiki yangu mkubwa sana anayeitwa Maganga, yeye alikutana na mimi na kunionyesha namna ya kujisajili na kucheza. Na baada ya hapo niliweza kucheza mwenyewe’’. Alisema John.
  Mimi katika michezo ya kubashiri ya Sportpesa nacheza aina moja tu ya mchezo ambao ni Jackpot. Na katika jambo hili la ubashiri sina utani wala maskhara hata kidogo. ‘’
  Huwa nacheza Jackpot tu. Na kwa siku ambapo Jackpot inatoka huwa nacheza mikeka kama saba au nane.
  Akielezea namna alivyopata ushindi huu wa Jackpot bonus anasema aliona mkeka wa jackpot siku ya Jumatatu na kuanza kucheza papo hapo. ‘’Sikusubiria cha Ijumaa wala cha Jumamosi, nilichagua timu zangu ninazoziamini muda ule ule nilipoziona timu, na baada ya hapo sikuzifuatilia’’.
  Anaendelea kusema alikuja kujua kashinda baada ya juzi kutaka kuongeza pesa na kuona haziingii ndipo alipotizama kwa makini akaona kama pesa ipo milioni 4.
  ‘’Kwa kweli sikuamini ila kwa kuwa nina imani na Sportpesa nilipiga simu Sportpesa kwakutumia namba za huduma kwa wateja na wakanithibitishia ni kweli nimeshinda na kunitaka nifike ofisini kwao kama unavyoniona hivi sasa’’.
  John anawashauri watanzania wote wasisite kucheza Jackpot ya Sportpesa kwani ndio njia sahihi na ya uhakika ya kushinda hela. ‘’ pamoja na kwamba kwa miaka yote minne tangu nimeanza kucheza sikuwahi kushinda chochote, mimi nilimtumainia Mungu na kuamini siku yangu itafika. Kama unavyoona siku yangu imefika kweli’’.
  Anamalizia kwa kusema fedha aliyopata atatoa fungu la kumi na nyingine atatumia kwenye ada na karo za shule za Watoto wake.
  Kwa wiki hii kiwango cha Jackpot hakijawahi kutokea kwani kipo 918,137,180.
  Kwa upande wa Sportpesa Meneja Uhusiano na Mawasiliano Sabrina Msuya alimpongeza sana John kwa ushindi wake na kumsihi ajitahidi hizo fedha azitumie vizuri maana ni pesa nyingi.
  “Hivi sasa Jackpot imepanda hadi shilingi 918,137,180 ambapo ndio kwa mara y akwanza kufika kiasi hicho tangu Jackpot ianze kutolewa”
  “Hiki ni kiasi kikubwa sana cha fedha na ninauhakika mshindi atakayeondoka nazo atakuwa ni mtu mwingine kabisa. Historia yake itabadilika na familia yake kwa ujumla”
  Kumbuka kwamba bado tunaendelea kutoa Jackpot bonus kila wiki kwa washindi watakaobashiri kwa usahihi mechi 10-12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FUNDI SELEMALA ASHINDA JACKPOT BONUS YA SPORTPESA. Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top