• HABARI MPYA

  Monday, February 07, 2022

  MAHREZ APOZA MACHUNGU YA AFCON MAN CITY


  MSHAMBULIAJI Riyad Mahrez jana aliweka kando machungu ya kushindwa kuisaidia Algeria kutetea taji la AFCON baada ya kufunga mabao mawili kuiwezesha Manchester City kuichapa Fulham 4-1 usiku wa Jumamosi Uwanja wa Etihad na kutinga Hatua ya 16 Bora Kombe la FA England.
  Mahrez alifunga dakika ya 53 kwa penalti na 57, wakati mabao mengine ya Man City yalifungwa na İlkay Gündoğan dakika ya sita na John Stones dakika ya 13, wakati bao pekee la Fulham lilifungwa na Fabio Carvalho dakika ya nne.
  Nayo Chelsea ililazimika kusubiri hadi dakika 120 kusonga mbele kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Plymouth Argyle Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Beki, Macaulay Gillesphey alianza kuifungia Plymouth Argyle dakika ya nane kabla y The Blues kutoka nyuma kwa mabao ya César Azpilicueta dakika ya 41 na Marcos Alonso dakika ya 105 na ushei.
  Naye Harry Kane jana alifunga mabao yote, Tottenham ikiichapa Brighton 3-1 na kutinga Raundi ya Nne ya Kombe la FA England. Bao pekee la Brighton lilifungwa na Yves Bissouma.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAHREZ APOZA MACHUNGU YA AFCON MAN CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top