• HABARI MPYA

  Thursday, February 10, 2022

  LUKAKU AIPELEKA CHELSEA FAINALI KOMBE LA DUNY


  BAO pekee la mshambuliaji Mbelgiji, Romelu Lukaku dakika ya 32 limeipa Chelsea ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Al Hilal katika mchezo wa Nusu Fainali Klabu Bingwa ya Dunia usiku wa Jumatano Uwanja wa Mohammed Bin Zayed Jijini Abu Dhabi, Saudia Arabia.
  Sasa mabingwa hao wa Ulaya watamenyana na Palmeiras ya Brazil katika Fainali Jumamosi baada ya Mabingwa hao wa Amerika Kusini kuitoa Al Ahly ya Misri.
  Kwa upande wao, mabingwa wa Asia, Al Hilal watawania nafasi ya tatu dhidi ya mabingwa wa Afrika, Al Ahly Jumamosi pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LUKAKU AIPELEKA CHELSEA FAINALI KOMBE LA DUNY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top