• HABARI MPYA

  Thursday, February 17, 2022

  BEKI WA ZAMANI SIMBA AFARIKI DUNIA


  BEKI wa zamani wa Simba, Adam Suleiman ’Tata’ amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwao, Tanga ambako alirudishwa kutoka Morogoro alipokuwa anaishi baada ya hali yake kuwa mbaya.
  Adam Suleiman aliyeibukia Muheza Shooting akacheza pia na Reli ya Morogoro ni baba wa beki mwingine wa Simba, Miraj Adam ambaye alifuata nyayo za baba yake kwa kucheza Msimbazi.
  Adam Suleiman alicheza Simba mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanawe aliibukia timu ya vijana ya Simba mwaka 2012, kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa mwaka 2013, lakini baada ya misimu miwili akaachwa.
  Marehemu Adamu Seleman (wanne kushoto) aliyechuchumaa kwenye kikosi cha Simba mwaka1989.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  1 comments:

  Anonymous said... February 19, 2022 at 9:06 AM

  Best online baccarat machines for Android
  Baccarat. Baccarat Online, Real Money, 파라오 바카라 Online Casino. If you 우리 카지노 총판 모집 are new to the game, this 온라인 라이브 카지노 is definitely a worthy game. 우리 카지노 더킹 It is one of the most played casino games santiyepazari.com

  Item Reviewed: BEKI WA ZAMANI SIMBA AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top