• HABARI MPYA

  Sunday, February 20, 2022

  MAN UNITED YAICHAPA LEEDS 4-2 ELLAND ROAD


  TIMU ya Manchester United imepata ushindi wa ugenini wa 4-2 dhidi ya Leeds United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Elland Road.
  Mabao ya Man United yamefungwa na Harry Maguire dakika ya 34, Bruno Fernandes dakika ya 45, Fred dakika ya 70 na Anthony Elanga dakika ya 88 wakati ya Leeds yamefungwa na Rodrigo dakika ya 53 na Raphinha dakika ya 54.
  Kwa ushindi huo, Man United inafikisha pointi 46 katika mchezo wa 26 na kurejea nafasi ya nne, wakati Leeds inabaki na pointi zake 23 za mechi 24 katika nafasi ya 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAICHAPA LEEDS 4-2 ELLAND ROAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top