• HABARI MPYA

  Saturday, February 12, 2022

  PETER APIGA HAT TRICK AZAM YASHINDA 6-0


  WENYEJI, Azam FC wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 6-0 dhidi ya Baga Friends ya Bagamoyo usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na washambuliaji Mzambia, Justin Zulu kwa penalti dakika ya 15, mzawa Paul Peter matatu dakika za 18, 20 na 44, kiungo Mzambia, Paul Katema dakika ya 54 na beki Mghana, Daniel Amoah dakika ya 89.
  Katika mchezo uliotangulia, Geita Gold walikuwa wa kwanza kwenda Robo Fainali baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbuni FC, bao pekee la George Mpole dakika ya tatu Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PETER APIGA HAT TRICK AZAM YASHINDA 6-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top