• HABARI MPYA

  Friday, February 25, 2022

  GEITA, NAMUNGO ZAFUNGUA MZUNGUKO WA PILI KWA SARE


  WENYEJI, Geita Gold wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC katika mchezo wa kwanza kabisa wa duru la pili Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
  Geita Gold walitangulia kwa bao la George Mpole dakika ya 73, hilo likiwa bao lake la nane la msimu, kabla ya Iddi Farjala kuisawazishia Namungo FC dakika ya 84.
  Kwa sare hiyo, Namungo FC inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 16, ikizidiwa wastani wa mabao tu na Azam FC zikifuatana nafasi ya tatu na ya nne, wakati Geita Gold inafikisha pointi 21 mechi 16 nafasi ya sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA, NAMUNGO ZAFUNGUA MZUNGUKO WA PILI KWA SARE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top