• HABARI MPYA

  Sunday, February 27, 2022

  ABRAMOVICH AJIWEKA KANDO UENDESHAJI CHELSEA


  MMILIKI wa Chelsea, Roman Abramovich amekabidhi usimamizi na uendeshaji wa klabu yake hiyo kwa taasisi ya hisani, kuonyesha  amekataa wito wa kumtaka aachie ngazi kufuatia nchi yake, Urusi kuivamia Ukraine.
  Bilionea huyo ambaye amekuwa mmiliki wa Chelsea tangu mwaka 2003, hajatoa tamko lolote juu ya vita huyo.
  Abramovich amewekeza kiasi cha zaidi ya dola za Kimarekani Bilioni 2  Chelsea, na kuifanya klabu hiyo na mafanikio Zaidi England.
  Tangu Abramovich aichukue Chelsea imeshinda mataji 19 jumla na ndio mabingwa wa sasa Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ABRAMOVICH AJIWEKA KANDO UENDESHAJI CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top