• HABARI MPYA

  Sunday, February 20, 2022

  KMC YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0 DAR


  MABAO ya Awesu Awesu dakika ya 68 na Salum Kabunda dakika ya 90 na ushei yameipa KMC ushindi wa 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, KMC inafikisha pointi 19 katika mchezo wa 15 na kusogea nafasi ya tisa, wakati Dodoma Jiji inabaki na pointi zake 17 za mechi 15 katika nafasi ya 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top