• HABARI MPYA

  Saturday, February 26, 2022

  MTIBWA SUGAR YAICHAPA MBEYA KWANZA 2-1 SOKOINE


  TIMU ya Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Mbeya Kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Mayanja Mululi dakika ya 38 na Omary Sultan dakika ya 75, wakati la Mbeya Kwanza limefungwa na Habib Kyombo kwa penalti dakika ya 41.
  Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 15 na kusogea nafasi ya 13, wakati Mbeya Kwanza inabaki na pointi zake 13, ikishukia nafasi ya 15 katika ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAICHAPA MBEYA KWANZA 2-1 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top