• HABARI MPYA

  Sunday, February 27, 2022

  MBEYA CITY YAICHOMOLEA PRISONS JIONI KABISA, 1-1


  TIMU za Tanzania Prisons na Mbeya City zimegawana pointi baada ya sare ya 1-1 jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Adili Buha alianza kuifungia Prisons dakika ya saba, kabla ya Ssemuju Joseph kuisawazishia Mbeya City dakika ya 86.
  Kwa sare hiyo, Mbeya City inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 16, ingawa inabaki nafasi ya tano, ikizidiwa tu wastani wa mabao na Azam FC ambayo pia ina mechi moja mkononi.
  Hali ni mbaya kwa Tanzania Prisons ambayo baada ya sare ya leo inafikisha pointi 12 katika mchezo wa 16 na kuendelea kuzibeba timu nyingine 15 kwenye Ligi Kuu.
  Mechi iliyotangulia mchana wa leo,  wenyeji, Ruvu Shooting wamelazimishwa sare ya 1-1 pia na Dodoma Jiji FC Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
  Waziri Junior alianza kuifungia Dodoma Jiji dakika ya 11, kabla ya Abrahman Mussa kuisawazishia Ruvu Shooting dakika ya 58.
  Ruvu Shooting inafikisha pointi 16 katika mchezo wa 16 na kurejea nafasi ya 12, wakati Dodoma Jiji wanafikisha pointi 18 katika mchezo wa 16 na kusogea nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAICHOMOLEA PRISONS JIONI KABISA, 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top