• HABARI MPYA

    Tuesday, February 22, 2022

    NAMUNGO FC YAICHAPA MBEYA CITY 2-0 ILULU


    WENYEJI, Namungo FC jana wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
    Mabao ya Namungo FC yamefungwa na Lucas Kikoti dakika ya 40 na Relliant Lusajo dakika ya 48 na kwa huo wanafikisha pointi 23 na kumaliza mechi ya 15 za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu katika nafasi ya nne, wakiziwa moja tu na Azam FC inayoshika nafasi ya tatu ikiwa na mechi moja mkononi pia.
    Mbeya City inabaki na pointi zake 23 za mechi 15 pia nafasi ya tano.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NAMUNGO FC YAICHAPA MBEYA CITY 2-0 ILULU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top