• HABARI MPYA

  Friday, February 25, 2022

  ARSENAL YAICHAPA WOLVES 2-0 EMIRATES


  WENYEJI, Arsenal wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Wolverhampton Wanderers katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Hwang Hee-chan aliifungia Wolves bao la kuongoza dakika ya 10, kabla ya Arsenal kutoka nyuma kwa mabao ya Nicolas Pepe dakika ya 82 na Alexandre Lacazette aliyemlazimisha Jose Sa kujifunga dakika ya 90 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 45 katika mchezo wa 24 na kusogea nafasi ya tano ikizidiwa pointi moja na Manchester United ambayo hata hivyo imecheza mechi moja zaidi, wakati Wolves inabaki na pointi zake 40 za mechi 25 nafasi ya saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAICHAPA WOLVES 2-0 EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top