• HABARI MPYA

  Sunday, February 06, 2022

  SIMBA SC YAILAZA MBEYA KWANZA 1-0 BAO LA CHAMA


  BAO pekee la kiungo Mzambia, Clatous Chama dakika ya 80 limetosha kuipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya Kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. 
  Sifa zimuendee mshambuliaji Mnyarwanda, Meddie Kagere aliyevunja mtego wa kuotea wa mabeki wa Mbeya Kwanza na kuendeleza shammbulizi lililozaa bao hilo.
  Kwa ushindi huo, mabingwa hao watetezi wanafikisha pointi 31 katika mchezo wa 14, ingawa inabaki nafasi ya pili, ikizidiwa pointi tano na watani wa jadi, Yanga ambao pia wana mechi moja mkononi.
  Mbeya Kwanza wanabaki na pointi zao 13 za mechi 14 pia katika nafasi ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAILAZA MBEYA KWANZA 1-0 BAO LA CHAMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top