• HABARI MPYA

  Tuesday, February 15, 2022

  MAKONGORO KATIBU WA ZAMANI YANGA AFARIKI DUNIA


  ALIYEWAHI kuwa Katibu Mkuu klabu ya Yanga miaka ya 1980, Issa Makongoro amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
  Kwa mujibu wa taarifa ya familia yake zinasema msiba uko Mikocheni kwa Warioba na maziko yatafanyika leo Makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.
  Uongozi wa Yanga SC umesema umepokea kwa msikitiko makubwa taarifa ya msiba wa kiongozi wake huyo wa zamani, enzi za mfumo wa Makatibu wa kuchaguliwa kwa kura za wachama, tofauti na sasa watendaji wa nafasi hizo wanaajiriwa. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAKONGORO KATIBU WA ZAMANI YANGA AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top