• HABARI MPYA

  Friday, February 11, 2022

  BEKI WA TAIFA STARS AFCON 2019 AFARIKI DUNIA  BEKI wa zamani wa Yanga SC na timu ya taifa ya Tanzania, Ally Abdulkarim Ibrahim Mtoni ‘Sonso’ (28) amefariki dunia leo wakati akikimbizwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
  Sonso aliyezaliwa Machi 13, mwaka 1993 Jijini Dar es Salaam, alikuwa nje ya Uwanja kwa muda baada ya kuumia mguu kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba Novemba 19 mwaka jana Ruvu Shooting ikichapwa 3-1 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
   
  Chanzo haswa cha kifo cha marehemu au maradhi yaliyokuwa yakimsumbua zaidi ya maumivu ya mguu hakijaelezwa ila mazishi yake yatafanyika nyumbani kwao, Kondoa Magomeni Jumamosi.
  Mtoni alisajiliwa Yanga akitokea Lipuli ya Iringa msimu wa 2019-2020 kabla ya kuachwa baada ya kuachwa msimu uliofuata akaenda Kagera Sugar ambako aliichezea hadi msimu huu alipojiunga na Ruvu Shooting.
  Ally Sonso alikuwemo kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichoshiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Misri mwaka 2019.
  Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Ally Mtoni Sonso. Amin.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEKI WA TAIFA STARS AFCON 2019 AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top