• HABARI MPYA

  Wednesday, February 23, 2022

  YANGA SC YAWAPIGA MTIBWA 2-0 MANUNGU


  VIGOGO, Yanga SC wamekamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar jioni ya leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
  Mabao ya Yanga leo yamefungwa na kiungo Mrundi, Saido Ntibanzonkiza dakika ya 45 na ushei na mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele dakika ya 66.
  Kwa ushindi huo, Yanga inakamilisha mechi 15 za mzunguko wa kwanza wa ligi na pointi 39, nane zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao pia wamecheza mechi 15.
  Mtibwa Sugar baada ya kipigo cha kwanza nyumbani, Manungu msimu huu wanabaki na pointi zao 12 za mechi 15 nafasi ya 15 Ligi ya timu 16, ambayo mwishowe mbili zitateremka moja kwa moja na mbili kwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kusalia Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAWAPIGA MTIBWA 2-0 MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top