• HABARI MPYA

  Sunday, February 06, 2022

  CAMEROON YASHINDA NAFASI YA TATU AFCON

  WENYEJI, Cameroon jana wametoka nyuma kwa mabao 3-0 na kushinda kwa mikwaju ya penalti 5-3 dhidi ya Burkina Faso katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu Kombe la Mataifa ya Afrika Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaounde.
  Burkina Faso ilitangulia kwa mabao ya Steeve Farid Yago dakika ya 24, kipa Andre Onana aliyejifunga dakika ya 43 na Djibril Ouattara dakika ya 49, kabla ya Cameroon kuzinduka kwa mabao ya Stéphane Cédric Bahoken dakika ya 71 na Vincent Paté Aboubakar mawili, dakika ya 85 na 87.
  Waliofunga penalti za Cameroon ni Vincent Aboubakar, Nicolas Ngamaleu, Karl Brillant Toko Ekambi, Pierre Kunde Malong na Ambroise Oyongo Bitolo, wakati waliofunga za Burkina Faso ni Issa Kaboré, Soumaila Ouattara na Steeve Farid Yago, huku Ibrahim Blati Toure akikosa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAMEROON YASHINDA NAFASI YA TATU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top