• HABARI MPYA

  Sunday, February 27, 2022

  MAYELE ATETEMA MARA MBILI, YANGA YASHINDA 3-0
  VINARA, Yanga SC wameuanza vyema mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Kagera Sugar usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga SC leo yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele mawili dakika ya 30 na 50 na kiungo Mrundi, Saido Ntibanzokiza dakika ya 64.
  Yanga ingeweza kuondoka na ushindi mnoni zaidi kama si wachezaji wake, Mayele, Ntibanzokiza na mtokea benchi, mshambuliaji Mkongo mwingine, Heritier Makambo kupoteza nafasi nzuri za kufunga.


  Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 42 katika mchezo wa 16 na kutanua uongozi wake kwa pointi 11 zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi.
  Kagera Sugar baada ya kupoteza mechi ya leo, wanabaki na pointi zao 20 za mechi 16 sasa katika nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE ATETEMA MARA MBILI, YANGA YASHINDA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top