• HABARI MPYA

  Wednesday, February 09, 2022

  TFF KUWAFANYIA SEMINA MAREFA WA LIGI KUU


  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) litaendesha semina ya siku tatu kwa marefa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kuanzia Februari 15, mwaka huu ili kutazama na kupitia changamoto kwa lengo la kuboresha katika maeneo mbalimbali.
  Taarifa ya TFF imesema huu ni utaratibu wa kawaida kuwape semina waamuzi ili kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na washiriki watakuwa waamuzi wote wa Ligi Kuu pamoja na Kamati ya Waamuzi.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF KUWAFANYIA SEMINA MAREFA WA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top