• HABARI MPYA

  Monday, February 21, 2022

  SIMBA NA PAMBA, YANGA NA GEITA ROBO FAINALI ASFC


  MABINGWA watetezi, Simba SC watamenyana na Pamba FC ya Mwanza katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup ( ASFC), wakati watani wao, Yanga watamenyana na Geita Gold.
  Mechi nyingine za Robo Fainali ni Azam FC na Polisi Tanzania na Coastal Union dhidi ya Kagera Sugar.
  Mshindi kati ya Simba SC na Pamba FC atamenyana na mshindi kati ya Yanga na Geita Gold katika Nusu Fainali na mshindi kati ya Azam FC na Polisi Tanzania atakutana na mshindi kati ya Coastal Union na Kagera Sugar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA NA PAMBA, YANGA NA GEITA ROBO FAINALI ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top