• HABARI MPYA

  Wednesday, February 16, 2022

  SIMBA SC YATINGA ROBO FAINALI ASFC KIBABE HASWA


  MABINGWA watetezi, Simba SC wametinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa kishindo baada ya ushindi wa 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na Nahodha, John Bocco mawili dakika ya pili n 40, Clatous Chama matatu dakika ya 23, 25 na 73, Masinda aliyejifunga dakika ya 44 na Jimson Mwanuke dakika ya 70.
  Timu nyingine zilizofuzu Robo Fainali ni Azam FC iliyoichapa Baga Friends 6-0, Geita Gold iliyoichapa Mbuni FC 1-0, Coastal Union iliyoichapa Mtibwa Sugar 2-0, Kagera Sugar iliyoilaza Namungo FC 1-0, Polisi Tanzania iliyoipiga Tanzania Prisons 2-0, Yanga SC iliyolaza Biashara United 2-1 na timu pekee isiyo ya Ligi Kuu, Pamba ambayo imeitoa Dodoma Jiji FC.
  Droo ya Robo Fainali itafuatia wiki ijayo na mechi za hatua hiyo ya Nane Bora zitachezwa mwezi ujao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATINGA ROBO FAINALI ASFC KIBABE HASWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top