• HABARI MPYA

  Thursday, February 10, 2022

  DJIGUI DIARRA TAYARI KUREJEA KAZINI YANGA NA BIASHARA


  MLINDA mlango wa kimataifa wa Mali, Djigui Diarra akiwa mazoezini na klabu yake, Yanga SC baada ya kurejea nchini kutoka nchini Cameroon alipokuwa na timu yake ya taifa kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zilizomalizika Jumapili kwa Senegal kuwa mabingwa.


  Baada ya kukosekana tangu mwishoni mwa Desemba, Diarra anatarajiwa kuonekana tena kazini Yanga ikimenyana na Biashara United katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) Jumanne Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DJIGUI DIARRA TAYARI KUREJEA KAZINI YANGA NA BIASHARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top