• HABARI MPYA

  Wednesday, February 09, 2022

  KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA LIVE STAR TIMES


  KAMPUNI ya Star Times Tanzania, imetangaza kurusha  moja kwa moja (Live) michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kwa hatua za makundi, inayoanza kutimua vumbi Februari 12.                                           akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa masoko na maudhui David Malisa,  alisema kuwa lengo la Star Times kurusha michuano hiyo ni kujali Watanzania wapendwa michezo.                "Leo tutafanya uzinduzi huu wa michuano ya mpira wa miguu wa Federation Cup (kombe la shirikisho Afrika) kupitia kisimbuzi cha startimes".                        "Kwakuwa StarTimes tunawajali wateja wetu wasipitwe na mambo mazuri, tunazidi kuwapa burudani mara 100 zaidi kama kampeni yetu ya mwaka huu inavyosema, kwa mara ya kwanza tunawaletea michuano hii ya kombe la shirikisho Afrika ambayo itaanza kuonekana rasmi kuanzia siku ya Jumapili"alisema Malisa.                           Alisema kuwa  habari nzuri zaidi ni kwamba Michuano hiyo itaonyeshwa LIVE kupitia Chaneli ya TV3 tena kwa lugha ya Kiswahili, katika kisimbuzi  cha Startimes.                                                                         "Kwa watumiaji wa Dish chaneli ya TV3 inapatikana kupitia chaneli namba 197 na kwa watumiaji wa Antenna kupitia chaneli namba 131, Ninachowasishi watazamaji wetu na wateja wetu wapendwa ni kulipia kifurushi cha Smart (Dish)kwa shilingi 21,000 tu mwezi mzima ama kwa watumiaji wa Antenna kulipia kifurushi cha Mambo kwa shilingi 15,000 tu mwezi m zima ili uone LIVE michuano hii hasa chama la wana Simba wakijitutumua. Hii ni nafasi kwako wewe kujiunga na familia ya StarTimes ili uweze kufurahia vipindi bora, chaneli bora kwa vifurushi vya gharama nafuu kabisa".                       Malisa alisema katika michuano hiyo itakuwa na Wadau mbalimbali wa Michezo  Antonio Nugaz, ambaye atakuwa sehemu ya uchambuzi.                                     Akizungumzia michuano hiyo Mkurugenzi wa TV3 Ramadhan Msemo, alisema kuwa wapenzi wa soka nchini watarajie mambo mazuri, maana wataonyesha mechi zote za michuano hiyo.                                                          alisema kwa Tanzania imepata bahati kuwa na mwakilishi ambaye ni Simba, ambapo Jumapili itacheza mechi yake ya kwanza ya hatua hiyo dhidi ya Asec Mimi's, utakaofanyika kwenye Uwanja wa Mpaka Jijini Dar es Salaam.                           "Wapenzi wa Soka watapata burudani hiyo kwa mechi zote za michuano hiyo iwe mechi ya ugenini na nyumbani" alisema Msemo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA LIVE STAR TIMES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top