• HABARI MPYA

  Saturday, February 26, 2022

  MAN UNITED YAAMBULIA POINTI MOJA KWA WATFORD


  WENYEJI, Manchester United wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Watford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford.
  Man United inafikisha pointi 47 baada ya sare hiyo katika mchezo wa 27, ikiendelea kushika nafasi ya nne kwa pointi mbili zaidi ya Arsenal ambayo hata hivyo ina mechi tatu mkononi.
  Kwa upande wao, Watford wanafikisha pointi 19, ingawa inabaki nafasi ya 19, ikiizidi pointi mbili tu Norwich City inayoshika mkia baada ya timu zote kucheza mechi 26.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAAMBULIA POINTI MOJA KWA WATFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top